Jumanne 16 Septemba 2025 - 01:04
Chaneli 13 ya Israeli: Israel inakabiliwa na “tsunami ya kisiasa” na upweke wetu baada ya kushindwa kwa shambulizi letu dhidi ya Qatar unaongezeka

Hawza/ Chaneli 13 ya Israeli imefichua kuhusu mgogoro mkubwa wa kisiasa na kidiplomasia unaoikumba Israel baada ya kushindwa kwa shambulizi dhidi ya Qatar na kuongezeka kwa upweke wa kimataifa.

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, Chaneli 13 ya Israeli imefichua kuhusu mgogoro mkubwa wa kisiasa na kidiplomasia unaoikumba Israel baada ya kushindwa kwa shambulizi dhidi ya Qatar na kuongezeka kutengwa kimataifa.

Chaneli 13 ya Israeli imeeleza yale ambayo Israel inakabiliwa nayo kwa sasa kama “tsunami ya kisiasa,” na ikabainisha kwamba upweke wa utawala huu baada ya “shambulizi lililofeli dhidi ya Qatar” umeongezeka.

Chaneli hii ya Israeli imeongeza kwamba: Nchi ambazo hapo awali zilijiona marafiki wa Israel na zingeweza kuwa na mustakabali wa pamoja nayo, kama vile Saudi Arabia, Misri na Jordan, sasa zinajikurubisha zaidi na Iran, na hazina tena imani ya kuwa Israel ni mshirika wa kuaminika.

Chaneli 13 ya Israeli, kwa kusisitiza kwamba hakika kuna tatizo la kidiplomasia hapa, imebainisha kwamba bado hatujajadili athari za upweke wa Israel ndani ya Umoja wa Mataifa.

Ni jambo la kutajwa kwamba shambulizi la Israel mjini Doha, ambalo lilikuwa jaribio la kuwalenga viongozi wa Hamas, liligonga mwamba na kusababisha idadi ya waliouawa na kujeruhiwa, Shambulizi hili pia lilikemewa kwa upana katika ngazi ya kimataifa na katika ulimwengu mzima wa Kiarabu.

Katika muktadha huu, mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Kiarabu na Kiislamu, katika kikao cha dharura kilichofanyika Jumapili, walisisitiza kwamba usalama wa Qatar “ni sehemu isiyotenganishwa na usalama wa kitaifa wa Kiarabu na Kiislamu.”

Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar, kwa kusisitiza kwamba ukiukaji endelevu wa sheria za kimataifa wa Israel katika shambulizi la kinyama mjini Doha ulikuwa dhahiri, walibainisha kwamba tendo hili haliwezi kuelezewa ila ni ugaidi wa kiserikali.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha